matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Apr 21, 2012

PINDA KUTOA TAARIFA YA KIKAO JUMATATU- KUSUKA AMA KUNYOA KWA MAWAZIRI WA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO

Prime Minister:  "Aisee jana na leo jasho limenitoka, yani wewe mwanangu zitto unataka kunitoa nishai mbele ya umma mh"
Zitto: "Hapana hapana mzee sio hivyo mkuu. Unajua wakati mwingine kukumbushana ni muhimu sana kwani bila hivyo hao watendaji wasingejikosoa. nafikiri nime play part yangu vizuri"
Hamad: "Tehe tehe tehe mimi sina la kusema Mkuu si unakumbuka hata mimi niling'olewa ila nikanusurika tu. ni ubishi tu hapa. ila mzee tupo pamoja katika hili"
 Mnyika: "hata leo nilipokuwa nasema jambo dogo tu la kurekebisha kipengele aisee nilishambuliwa mh we acha tu zitto. eti jamaa wanataka gati fasta fasta hivi wanadhani hii mikopo ya china ina riba ndogo. ni zaidi ya asilimia 70 sasa hii tutakuwa tunajenga ama tunabomoa. bora tuchelewe tufike. Mkuu si unajua ule  msemo kawia ufike"
Prime Minister: "Ninyi vijana kweli mmefanya niamke. kweli ninazeeka tu huu mwili ila naamini maini hayazeeki. Sitawaangusha tena tuvumiliane ni mapito tu haya. yatapita..............."

Kufuatia sakata la kamati za bunge kusoma ripoti zao imesemekana kuwa mawaziri kadha jana wameamua kuachia ngazi. habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa wengi wao wamejitoa muhanga ili kumuokoa waziri mkuu na kulinda heshima zao. hii inatokana na pale ambapo mbunge Zitto Kabwe alipotoa hitimisho la kamati zote ambapo alitoa mapendekezo ya kutafuta saini za wabunge 70 ama zaidi ili kufikisha asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kuleta hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. mapenda leo Mh Spika mama Makinda alitoa ufafanuzi kuwa hoja ya Zitto kamwe haiwezi kutendwa kwenye bunge hili kwani ilimlazimu afanye hivyo siku 14 kabla ya kuwasilisha. sasa vitendawili na sintofahamu vimebaki kwa watu ambapo haijulikani ni kwa nini wabunge wa CCM walikwenda kufanya vikao mbalimbali kuanzia juzi ili kunusuru hali hii.
Hata hivyo blog hii imemsikia Zitto akisema yeye hana uhakika kama maamuzi ya wana CCM ni kuwaengua mawaziri ama la. na pia ikumbukwe leo mheshimiwa waziri mkuu akitoka bungeni alisema kuwa hayuko tayari kuzungumza chochote hadi siku ya jumatatu ambapo bunge la jamuhuri litahairishwa hadi kikao kijacho.
Tunasubiri jumatatu tuone yatakayojiri..........................

Endapo watajiuzulu mawaziri kadhaa basi yafuatayo ni baadhi ya magazeti yakionyesha utabiri wao..




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge, John Mnyika wa Ubungo (kushoto), Kabwe Zitto wa Kigoma Kaskazini  na Hamad Rashid wa Wawi, kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 21, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...