matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Sep 28, 2013

JOHN LISU TENA KUJA NA DVD YA LIVE. NI PALE CCC UPANGA TAR 6 OCTOBER 2013



Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Tanzania ,John Lisu October 6 mwaka huu 2013 anatarajia  kurekodi tena album ya pili yenye jina "UKO HAPA "itakayo rekodiwa katika Ukumbi wa kanisa la City Christian Center  (CCC) Upanga jijini Dar es salaam album ambayo inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika muziki wa injili nchini Tanzania na kutoa hamasa kwa waimbaji wengine na kwaya mbalimbali kuanza kupenda kufanya kazi zinazorekodiwa LIVE.

  Mwanamuziki John Lissu ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Singida,Tanzania ni kijana aliyejaaliwa sauti ya ajabu, alianza kujulikana alipofanya album yake live ya 'Jehovah yu hai' ambayo inanyimbo nzuri sana na album ya kwanza kurekodiwa LIVE yaani audio na Video kwa pamoja. 


JUU:MAVAZI YA SIKU HIYO YA UZINDUZI YATAFANANIA HIVI

John Lisu amesema kuwa albam hii pili yenye jina  "Uko Hapa" ina jumla ya Nyimbo 11 ambazo zitarekodiwa live siku hiyo pia ameongeza kua aliamua kuipa jina albam hiyo la "Uko Hapa" kwa sababu kila wakati ambapo Lissu amekuwa akihudumu Mungu amekuwa hapo akihudumia watu wake.

CHINI:  John Lisu akiwa na timu yake katika maandalizi ya Live Recording ya Album yake mpya
Baada ya hapo amefanya kazi na kanisa la DPC akiwa mstari wa mbele kuongoza watu katika sifa na kuabudu. Alishiriki pia katika recording ya Sifa zivume, album nyingine iliyorekodiwa LIVE katika Ukumbi wa Mlimani City.

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...