matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Sep 25, 2013

WESTGATE KENYA SHOPPING MALL ULIVYOFANYIKA UGAIDI TUNAJIFUNZA NINI???



Ni kawaida nchini Kenya, hasa Nairobi, kukaguliwa wakati wa kuingia kwenye maduka makubwa ya maeneo mengine yenye mikusanyiko, lakini safari hii ukaguzi huo haukusaidia




JENGO LA WESTGATE LIKIFUKA MOSHI BAADA YA ASKARI NA VIKOSI KUPAMBANA NA MAGAIDI NDANI YA JENGO SIKU CHACHE ZILIZOPITA.



JUU: WATU WAKIOKOLEWA KUTOKA NDANI YA JENGO HILO LA WESTGATE

Jumamosi Septemba 21 ilikuwa siku ya kawaida kwa Wakenya wa matabaka mbalimbali. Wengi walibaki majumbani wakipumzika baada ya juma zima la kukurukakara za kutafuta riziki. Kwa wengine ilikuwa siku ya ujenzi wa taifa na walikwenda kazini kama kawaida.

Wengine waliamua kwenda kujivinjari katika sehemu mbalimbali za kujiburudisha. Hali haikuwa tofauti kwa wakazi wa eneo la Westlands ambalo ni sehemu inayohusishwa na walala hai.





West Gate, kwa miaka mingi, imekuwa mahali pa mabwenyenye na wageni kutoka nje wanaofanya kazi katika mashirika makubwa makubwa kama vile Umoja wa Mataifa hujiburudisha huku wakinunua wanachotaka. Ina maduka mengi makubwa pia imejengwa katikati ya mitaa ya kifahari.

Siku hiyo, muda wa saa sita  na nusu mchana Kituo cha Televisheni cha Nation  (NTV) kilitangaza kwamba kumekuwa na tukio la uhalifu West Gate. Kadiri saa ziliposonga ndipo ikadhihirika kwamba kumbe si wizi bali shambulizi la kigaidi.

Kuanzia hapo, tukio hilo likaanza kuvutia vituo vingine vya habari vilivyofunga virago vyao kuelekea huko ili vipeperushe habari za moja kwa moja kutoka eneo la tukio.

Kisa hiki ambacho sasa kimewaua takriban watu 62  kimeshangaza dunia na kuvishtukiza vikosi vya ulinzi vya Kenya.

Wavamizi wamejitambulisha katika mitandao ya kijamii kama vile Twitter kuwa ni waasi wa kundi haramu la Al-Shabaab na wanalipiza kisasi cha uvamizi wa majeshi ya Kenya Somalia. Kituo cha Televisheni cha Al-Jazeera kilikuwa kituo cha kwanza cha habari kutangaza kwamba waliofanya uvamizi huo ni Al-Shabaab.

Baada ya saa 24 na nne tangu uvamizi huo ufanyike, vikozi vya ulinzi vya Kenya (KDF) vilivamia jengo hilo Jumapili na wakawaokoa mateka wengi. Hata hivyo, bado kulikuwa kuna watu wazima  na watoto waliokuwa ndani wakihangaishwa na watekaji nyara hao wapatao 15.

Walioshuhudia kisa hicho wanasema kwamba, wavamizi waliingia jengo hilo baada ya kurusha maguruneti na kuwamiminia risasi walinzi na watu waliokuwa wakinunua bidhaa.

Baadhi ya viongozi waliowasili katika eneo hilo kujionea yaliyokuwa yakiendelea, ni aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga na Seneta Moses Wetangula. Viongozi hao walihutubia taifa wakisema kwamba tukio hilo limewaleta pamoja Wakenya bila kujali misingi ya kikabila au rangi.

KDF walipoingia jengo hilo, walifanikiwa kushika doria katika maeneo mbalimbali ambapo yaliweza kupata fursa nzuri ya kukabiliana na adui. Vikosi hivyo vilishirikiana na FBI ya Marekani, Mosad ya Israel na M16 ya Uingereza katika harakati hizo.
 
 
 Baada ya mashambulio ya kigaidi kwenye mall ya Westgate huko Nairobi, Peter Msechu amekuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kutoa wimbo maalum kwa ajili ya tukio hilo. Peter Msechu anasema kwamba kwa kutambua mchango watu wa Kenya kwenye muziki wake. Ameamua kutoa wimbo huu maalum kwa kuwafuta machozi wananchi wa taifa la Kenya.Sikila na download hapa

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...