matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Mar 23, 2011

VIDEO YA MIRIAM MAUKI IMEFANYWA KWA UJUZI WA HALI YA JUU MNO. NZURI SANA.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza uimbaji wake Miriam Lukindo(zamani) na sasa Miriam Mauki hakuwahi kutoa video yeyote ya muziki wake wa nyimbo zake. Tangu album ya kwanza iliyompa umaarufu mkubwa  mpaka hii ya 'ni asubuhi' hakuwahi kufanya shooting. mara nyingi amekuwa akionekana kwenye matamasha ya nyimbo za injili na ndipo sasa watu wengi walijiuliza ni kwa nini hakuwa kutoa video. ni hivi juzi tu wanamuziki wa nje waliiga nyimbo zake za kuabudu. nyimbo zilizompa umaarufu ni pamoja na ya 'niguse tena' ambao uliigwa na wanamuziki wa nje. nyimbo nyingine ni Amen Aimela ambao ulishika chat na ukamfanya kufahamika maradufu na kualikwa katika hafla mbalimbali za hapa tanzania na nje ya nchi. Ama kwa sasa video yake ipo hewani na ni ya ukweli. Walioaandaa video za miriam wanastahili kupewa pongezi kwa ujuzi wa kuandaa kwa ubora wa hali ya juu sana. Big up and to God be glory!!!!!!

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...