matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Jan 29, 2012

Daniel Makabali ni Moja kati ya producers wazoefu tanzania.


Watu wengi wanajiuliza kazi ambazo huwa zinasikika hewani kuwa zimerekodiwa na producer gani! Majibu ni haya. huyu jamaa anaitwa Daniel Makabali ambaye amefanya kazi nyingi sana za iyelele team chini ya Pius Senyagwa. kazi kama iyelele Yesu, maombi yangu, viva tanzania  na nyinginezo ambaz zinafanya vizuri sana radioni kiasi kwamba watu wengi wanaulizia mara kwa mara ni wapi kwa kuzipata. Dani makabali anafanya kazi zake katika studio maarufu jijini dar es salaam zinazoitwa "Omega Studio" pale mwananyamala. kwa mawasiliano zaidi unaweza kujiunga kwenye page yake kwenye facebook kama daniel makabali. sikiliza baadhi ya kazi hapa hapa kwenye blog yako uipendayo www.iyeleleteam.blogspot.com. Kihistoria ni kuwa producer huyu alianza kama mmoja wa wanamuziki katika bendi ya injili iliyojulikana kama SIFUNI BAND inayopatikana mjini dodoma. hatimaye akajiunga na studio moja iliyojulikana kama gc records huko dodoma. ndipo alipoamua kuja dar es salaam kwa kazi zaidi za kufanya production.

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...