Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini
Tanzania ,John Lisu October 6 mwaka huu 2013 anatarajia kurekodi
tena album ya pili yenye jina "UKO HAPA "itakayo rekodiwa katika Ukumbi
wa kanisa la City Christian Center (CCC) Upanga jijini Dar es salaam
album ambayo inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika muziki wa
injili nchini Tanzania na kutoa hamasa kwa waimbaji wengine na kwaya
mbalimbali kuanza kupenda kufanya kazi zinazorekodiwa LIVE.
JUU:MAVAZI YA SIKU HIYO YA UZINDUZI YATAFANANIA HIVI
Baada ya hapo amefanya kazi na kanisa la DPC akiwa mstari wa mbele kuongoza watu katika sifa na kuabudu. Alishiriki pia katika recording ya Sifa zivume, album nyingine iliyorekodiwa LIVE katika Ukumbi wa Mlimani City.