ANGALIA KIPANDE KIFUPI CHA VIDEO SIKU HIYO YA HARAMBEE HUKU CHOIR MASTER NI MWANZILISHI WA KUNDI HILO BWANA LUNGWA(MSTAAFU)
Uhondo wa ngoma uingie ucheze ndipo hapo usemi huu ulishika nafasi tarehe 6/10/2013 kanisa la anglican mjini dodoma ambapo kwaya kongwe inayojulikana kama kwaya uinjilisti uvuke ilipofanya harambee kwa ajili yakuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo mgahaw hapo kwenye mnara nje ya kanisa lao pamoja na duka la rejareja la kuuza kazi zao na kazi za wanamuziki wengine wa injili nchini. kwa mujibu wa mwenyekiti wa kwaya hiyo bwana Nico Ndaro amesema hivi karibuni watabuni miradi mbalimbali ambayo itakuwa ni mbadala wa kupata fedha tofauti na kutegemea mauzo ya cd na dvd peke yake.
wakati huu kundi hili limekuwa likialikwa sehemu nyingi sana ndani na nje ya nchi ili kutoa huduma/ hatahivyo wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kwa sababu ya uchumi wao kuwa mdogo. Maono haya ya kuanzisha miradi ni ya muda mrefu ambayo yamekuwa yakisuasua hatimaye kuamua kuanza kufanya harambee ya wenyewe kabla ya kushirikisha wadau wengine. Jumla ya zaidi ya shilingi 2,400,000/= ilikusanywa siku hiyo na pia kulitolewa mbuzi na nguruwe kwa ajili ya mnada jumapili itakayofuata ili kuendelea kufanya changizo.
Hawa ni viongozi wa sasa wa kund la Uvuke ambapo wa kwanza kulia ni mwenyekiti mwake na anayefuata ndiye msaidizi wa mwenyekiti
Hapo viongozi wakitoa michango yao kufanikisha shughuli yenyewe. ni sawa na kusema kwenye kikao cha harusi bwana harusi lazima aulizwe ana kiasi gani??!!?
NICO NDARO- MWENYEKITI AKIPIGA MAKOFI KUSAPOT
PIASON AMBAYE NI MLEZI WA KUNDI NA MWENYEKITI MSTAAFU AKITOA MCHANGO WAKE HAPA.
MAKUSANYO YAKIENDELEA KUFANYIKA KWA UANGALIFU KUTOKA KWA WANAKWAYA WENYEWE
MR YOBWA MC WA SIKU NYINGI SANA MZOEFU WA SHUGHULI KAMA HIZI NI MWIMBAJI WA KUNDI HILI NA MWALIMU WA MUDA MREFU SANA
NICCO NDARO MWENYEKITI KATIKA POZI LA PICHA AKIFURAHIA JAMBO
MUIMBAJI WA KUDUMU WA KUNDI HILI MR PIUS SENYAGWA AMBAYE KWA SASA NI BLOGGER NA MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI (SOLO ARTIST) ALILELEWA KATIKA KUNDI HILI HADI HAPO ALIPOFIKIA NAYE AKITOA MCHANGO WAKE HAPO KANISANI KWENYE HARAMBEE
MBEBA MAONO WA KUNDI HILI AMBAYE NDIYE MWANZILISHI MZEE LUNGWA AKITOA MCHANGO WAKE