Baada ya kupumzika kwa takribani miaka miwili toka wasimamishe ibada za kusifu na kuabudu siku za Ijumaa jioni, kundi la Glorious Worship Team (GWT) chini ya kiongozi wake Emanuel Mabisa kundi hilo limetangaza kuanza upya tena ibada hizo kuanzia ijumaa ya kwanza ya mwezi wa pili mwaka huu ingawa bado hawajatangaza mahali watakapokuwa wakifanyia maonyesho hayo awali kabla ya kusimamisha walikuwa wakifanyia katika ukumbi wa hoteli ya Atriums iliyopo Sinza jijini Dar es salaam.
Glorious Worship Team Kurejesha MOTIVATION FRIDAY.Kutokana na Maombi ya Watu wengi kumiss mitoko ya kiroho na kujikuta wanachanganyiwa habari na kudhani tumeanzisha vitu vingine, Hapana.Sisi Kama kawaida tunaendelea na Praise and worship ya Nguvu na vitu vingi kwa utukufu wa Mungu....inaanza mapema wiki ya kwanza ya Mwezi wa Pili! MD GWT"
Glorious ambao ni kundi la kwanza la muziki wa injili nchini kuamua kuwa na siku maalumu ya kuwakusanya mashabiki na wapenzi wa muziki wa injili kwa pamoja kila siku za ijumaa jioni ili kumsifu Mungu, kuchangamka na kucheza pamoja huku kundi hilo likisimamia ratiba nzima, utaratibu huo ulitokea kuanza kupendwa na wapendwa wengi ambao walikuwa wakiishia kujifungia ndani ya nyumba zao mpaka jumapili ndipo waende kanisani na kujikuta wakipata sehemu ya mtoko ambao hata hivyo ulikuja kusimama na sasa unarejea tena.
GWT mpaka sasa in a album mbili ya kwanza ilikuwa Niguse. SOURCE:rumaafrica blog