matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Jul 12, 2015

DK JOHN POMBE MAGUFULI ACHAGULIWA KUWA MGOMBEA WA URAIS WA JAMUHURI YA TANZANIA KWA TICKET YA CCM 12/07/2015

HATIMAYE HALMASHAURI KUU YA CCM IMEMTEUA KWA KURA 1,104 MH JOHN MAGUFULI AMBAYO NI SAWA NA ASILIMIA 87.1 YA KURA  ZOTE HALALI ZILIZOPIGWA


Tangu siku ya juzi yani tarehe 10/07/2015 kumekuwa na heka heka ndani ya chama cha mapinduzi ili kuweza kumchagua mgombea wake atakeyepeperusha bendera kwa niaba yake katika kutetea nafasi ya kiti cha urais ambacho kwa sasa kinakaliwa na Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa takribani miaka kumi sasa.
Leo tar 12/07/2015 hatimaye amepatikana Dk John Magufuli ambaye kwa sasa ni waziri wa ujenzi kama mgombea wa kiti cha uraisi 
Hata hivyo awali kabla ya kuchaguliwa kwake Mh Asha rose Migiro na Amina salum Ali ndio walioingia tatu bora pamoja na Dk Magufuli. 

 Amina Salum Ali


Asha Rose Migiro

Hata hivyo Dk John Magufuli alilazimika leo hii hii kumteua mgombea mwenza ambaye atakuwa naye kama makamu wa rais kama atachaguliwa na wananchi kutumika kama rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania hapo mwezi october mwaka huu wa 2015. Dk Magufuli alisikika akisema kwa kuwa mwaka huu chama cha ccm kimewapa kipaumbele zaidi wanawake hivyo hata yeye ametafakari kwa kina moyoni mwake na kuona kuwa ni bora apate mgombea mwenza mwanamke kuliko mwanaume. Hivyo alimteua mara moja Mh Samia Suluhu Hassan kama mgombea mwenza. Samia alionekana kama mwanamke shupavu sana ambaye mh Magufuli alimpendelea katika wadhfa huo.

 Samia Suluhu Hassan- mgombea mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya CCM.

Baada ya uteuzi huo hatimaye nderemo vifijo vilikuwa vikirindima katika mkoa wa dodoma pale ambapo mgombea huyu Dk Magufuli alipotambulisha majira ya jioni pale katika uwanja wa jamuhuri dodoma. Angalia matukio katika picha leo hii kutokea katika ukumbi wa convention wa CCM hadi uwanja wa jamuhuri dodoma..


Pichani ni mtumishi wa Mungu Tb Joshua wa nigeria akiwa na Familia ya Dk Magufuli pamoja na Janeth Magufuli ambaye ni mke wake na mtoto wao.
hii inaonyesha pia Dk Magufuli humtafuta Mungu. kwa kupewa mkono hapo ni ishara nzuri sana kwake. ni kama baraka za mvua zinamfuata. Tumuombee!!!









 spika Anna Makinda






 Pongezi





 first lady Salma Kikwete akimpongeza Janeth Magufuli


 Dk Magufuli na mgombea mwenza Samia Suluhu




UFUATAO baadhi ya WASIFU WA DK JOHN MAGUFULI
 
Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).
Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salfordnchini Uingereza.
Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanzaya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.
Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.
Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.
Mafunzo
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.
Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.
Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).
Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)
Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.
Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).
Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.
Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.

GENERAL
Salutation Hon. Member picture
First Name: Dr. John
Middle Name: Pombe Joseph
Last Name: Magufuli
Member Type: Elected Member
Constituent: Chato
Political Party: Chama Cha Mapinduzi
Office Location: P.O. Box 9144, Dar es Salaam




Office E-mail: jmagufuli@parliament.go.tz
Member Status: Active
Date of Birth 29 October 1959
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Chato Primary School CPEE 1967 1984 Primary School
Katoke Seminary Biharamulo, Kagera CSEE 1975 1977 Secondary School
Mkwawa High School ACSEE 1979 1981 Secondary School
Lake Secondary School ¿ Mwanza CSEE 1977 1978 Secondary School
Mkwawa College of Education Diploma in Education (Sc.) Chem., Maths&Edu. 1981 1982 Diploma
University of Dar es Salaam B.Sc Ed. (Hons) Chem.&Maths 1985 1988 Bachelor
Universities of Dar es Salaam, TZ &Salford -U.K. MSc. (Chem) 1991 1994 Masters Degree
University of Dar es Salaam. PhD (Chem) 2006 2009 PhD
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
UN-HABITAT Co-chair World Urban Forum (III) 2006 To Date
Ministry of Lands and Human Settlements Minister 2005 2/8/2008
World Road Congress (PIARC) 1st Delegate 2000 2005
Mtwara Development Corridor Member 2000 2005
Ministry of Works Minister 2000 2005
Ministry of Works Deputy Minister 1995 2000
Tanzania Chemical Society Member 1993 Todate
Nyanza Co-operative Union(NCU) Ltd.- Mwanza. Industrial Chemist 1989 1995
Sengerema Secondary School Teacher(Chemistry and Mathematics) 1982 1983
Ministry of Livestock and Fisheries Development Minister 13/02/2008 To Date
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi - CCM( Biharamulo East) Member of Parliament of Tanzania 1995 Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member 1977 Todate
PUBLICATIONS
Description Date
Mulokozi A. M.; Akwilapo, L.D.: Buchweishaija, J.; Magufuli J. P., and Kyobe, J. ¿Securing the Mechanism of the Decomposition of CaCO3 by the Thermodynamics of the Reaction¿, East and Southern Africa Environmental Chemistry Workshop, pp 71-83, 1st ¿ 5th December 2003, Dar es Salaam 5 Dec 2003
Magufuli, J. P., ¿Funding requirements for the EAC Road network project the East African Community Roads Development partners Consultative meeting 29th ¿ 30th April, 2003 Arusha Tanzania. 30 Apr 2003
Magufuli, J. P., (MP) PIARC First Delegate and Minister for Works of the United Republic of Tanzania.¿ Access to Mobility a basic Social Service, Special Trunk Roads project, Design and Build Tanzania model, XXIInd World Road Congress, 19 ¿ 25 October, 2003 Durban, South Africa. 25 Oct 2003
Mulokozi, A. M., Kyobe, Magufuli, J. P. and R. Whitehead. ¿A New Rate Equation for Solid State Decompositions and its application to the Decomposition of CaCo3. TCS Inaug. Conf. Proc., 11 ¿ 16 July, 1999, p162 ¿ 183. 16 July 1999
Magufuli, J. P., ¿Background of the Mtwara Development Corridor¿ Meeting of the head of States from Malawi, Tanzania, Zambia and Mozambique during the Rounding of the Mtwara Development Corridor, 15 December, 2004, Lilongwe ¿ Malawi. 15 Dec 2004


Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...