KWA KUMBUKUMBU NZURI KWAKO MDAU WA IYELELE TEAM BLOG ANGALIA HII HAPA KWANZA.
MCHUNGAJI NA ASKOFU JOHN KOMANYA WA CATHEDRAL OF JOY.
Hakika nyota imezimika hapa duniani kwa kuondokewa na mtumishi huyu wa Mungu. kulingana na maelezo yaliyotolewa ni kuwa John Komanya alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. alipelekwa hospitali ya Hindu mandal siku mbili nyuma kwa ajili ya matibabu hadi hapo mauti ilipomfika alfajiri ya saa kumi leo hapo hospital Hindu mandal jijini dar es salaam. Marehemu ameacha mke mmoja na watoto watatu.
Mungu ni mwema kwa kuwa heri wale wafao katika bwana. hakika watauona ukuu wa Mungu.
HAPA CHINI NI PICHA MBALI MBALI ZA MTUMISHI HUYU
alikuwa ni mtu wa vijana kwa kuwa hata yeye bado alikuwa ni kijana
John Komanya na mkewe
Akionyesha ishara ya utumishi wake kwa kushika kitabu cha neno la uzima
Mwanzilishi wa band maarufu sana hapa dar es salaam CO band akiwa na vijana wake wa band hiyo.
Huduma ikiendelea na watu wakibarikiwa
JOHN KOMANYA AKIWA NA MKE WAKE PICHANI
Taarifa
ambazo zimetufikia alfajiri ya leo na kisha kuthibitishwa punde,
zinaeleza kwamba Askofu Mkuu na mwanzilishi wa kanisa la Cathedral of
Joy (CoJ), Apostle John Komanya, amefariki dunia alfajiri ya saa kumi
kwenye hospitali ya HIndu Mandal, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mchungaji msaidizi wa kanisa hilo, Abel John Kigeli, ameieleza GK kwamba Apostle Komanya alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari pamoja na typhoid, na kwamba siku za nyuma alikuwa amelazwa Hospitali ya Muhimbili, ambapo alikuja kuruhusiwa baada ya kupata ahueni.
Siku mbili nyuma ndipo alipozidiwa tena na hivyo kupelekwa Hospitali ya Hindu Mandal, ambapo mauti yalimkuta hapo. Marehemu ameacha mke na watoto 3 ambao wako nchini Marekani, sehemu ambayo pia alikuwa akihudumu.
Kwa sasa ratiba za ibada ya kanisa la CoJ ambalo lipo Gogoni Kiluvya, zimehamishiwa kwa dada wa marehemu, Makoka, ambapo ibada huanza saa nne asubuhi.
GK itaendelea kukuletea taarifa mpya kwa kadri itakavyokuwa inazipata.
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, Jina la BWANA lihimidiwe. - See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2015/07/hivi-punde-apostle-john-komanya-afariki.html#sthash.TVOQKub0.dpuf