matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Jan 24, 2017

STARS THOMAS AWAONYA KINA DADA WANAMUZIKI

STARA THOMAS:
Msanii mkongwe wa muziki, Stara Thomas amedai moja kati ya sababu ambazo zinawafanya wasanii wa kike wapotee kwenye muziki ni kuendekeza mapenzi.
Muimbaji huyo amedai wasanii wengi wanashindwa kurudi kwenye biashara ya muziki kutokana na kukata kwa mitaji ya kuweza kufanya biashara hiyo kutokana na vitendo vyao kama ulevi pamoja na kuendekeza mapenzi.

“Kuna vitu vingi vinavyopelekea mtu kushuka kimuziki kwanza ni ‘mind set’ ya mtu mwenyewe lakini unajua mwanamke kama mwanamke ikifika mahali akiendekeza sana mapenzi lazima ashuke,” muimhaji huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Aliongeza, “Vilevile wanakula wengine unga, wanakunywa pombe sanaa kwa hiyo wanashindwa kuangalia biashara yao hiyo maana muziki sasa ni biashara, mara anakuja kushtukia msingi wake wa biashara hiyo umekata,”

Muimbaji huyo amekuwa kimya kwenye muziki kwa muda mrefu toka aachie wimbo ‘Shamba la matunda’ ambao alimshirikisha LineX. Pia ikumbukwe kashawahi kuimba nyimbo mbalimbali za injili.
Source : bongo5.com

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...