TUMEPAKUA HII YA NDOA:
HIVI NILISHAFUNDISHA HII?
IRENE MBOWE SAYS:
KESHO NITAKUWA NA SOMO AMBALO NI VERY SENSTIVE. SOMO NYETI SANA.
NIOMBEJE KWA AJILI YA MUME.
ILA ITAKUWA VIZURI KAMA NITAANZA NA SOMO HILI HAPA.
Unatamani Ndoa ama Harusi?
Yaani unataka Mume ama Harusi?
Ndoa ni Mume.
Harusi ni Sherehe.
Si ndio eeee.
Mh...Nikiangalia msichana anavyohangaikia harusi.
Kwanza kabla ya harusi anavyohangaikia uchumba...
Yani mna zile pozi zenu za engagement..
Kijana anapiga magoti anakuvika pete.
Kisha unapiga picha mkono wa pete unasambaza mitandao yoote.
Na maneno THANKS GOD I FOUND HIM. HUBBY TO BE.
Nikifanikiwaga kupna picha hizi huwa nashinda siku nzima kwenye profile ya mdada huyo mwenye hizo picha. Naanza kuangalia profile yake mwanzo mwisho.
Kisha nasema.
MUNGU MPE AKILI NJEMA HUYU MSICHANA ANAYEINGIA NDOANI.
Isiwe alitaka Harusi badala ya Ndoa.
Maana ni kama namuona atakavyopata kichaa cha Ndoa baada ya muda fulani ambao ni chini ya 5 yrs ndani ya ndoa.
Anayetaka HARUSI mara nyingi...
1. Hajali anaolewa na nani.
2. Hawezi na hayuko tayari kuhudumia Ndoa.
3.Divorce haimsumbui. Anaiishi.
Anayetaka NDOA Mara nyingi....
1.Anajali sana anaolewa na nani.
2.Anaweza na yuko tayari kuhudumia ndoa.
(Mpaka machozi yananilenga lenga)Najua huyu ni Mjeshi. I said. Mjeshi anapambanaga tu nyakati zote.
3.Hataki kusikia kitu kinaitwa Divorce.
MUNGU WASAIDIE WANAWAKE WOOTE WENYE UTAYARI WA NDOA.
***********
SEHEMU YA PILI
Matokeo mazuri ya ndoa bora yanategemea sana umeolewa na nani. Na wewe ni nani.
Biblia inasema Mwanamume atakutawala.
Mume ni mtawala.
Sasa najiuliza haraka tu. Unaingia kwa mtawala wa aina gani.
Maana Mtawala Bora ama kwa hakika Utawala wake unakuwa wa haki. Si ndio?
Ok ok. Juzi kati Mwl Mwakasege kafundisha habari ya MKUU ASIYE NA AKILI HUTESA WATU.
So Mume ni mkuu wa familia. Anapokuwa hana akili inakuwaje?????anatesa familia si ndio eee.
Ok ok. So unaolewa na nani?ndilo swali la msingi la kujiuliza.
Hapa na deal na wanaotaka Ndoa. Yaani Mume.
Wanaotaka harusi nitawasaidia kuwaambia best mc... best cake maker.. best salon na best mpambaji.
Ila kwa wanaotaka Ndoa naomba hili weka akilini nani anakuoa.
Juzi tumesoma habari ya SEX IS NOT LOVE.
Hii inahusika na mmeshaisoma.
Sasa nani wa kukuoa. Ndicho kingine.
Nikisoma mahali. Kwa Samuel Nathaniel Sasali. Sijui ni Insta ama hapa face book.
Aliongea vyema.
Kwamba wanandoa wanapoingia ndoani wanajua yanayowakabili?
Nusura nidondoshe chozi.
Nikasoma pale "Mkikosa watoto inakuwaje.. mkipata watoto walemavu inakuwaje.... mmoja akaugua inakuwaje?
NDIO MAANA NATAKA MKE UWE MJESHI. Hivi ndivyo vita vya kupambana navyo mke.
UNATAKA NDOA.
SIO???
Uwe na utayari. Kuhudumia ndoa. Wakati unaofaa na usiofaa.
Uwe tayari kujifunza UPENDO.
Maana unaingia sasa ndoani.
Anaweza kubadilika... ama la anaweza asiwe uliyemtegemea... what next?
Anayeolewa na kuishi Divorce hii haimsumbui kabisa. Its easy.
Wewe ukiuliza watumishi gani wanaweza kunipa msaada wa maombi yeye anauliza who is the best lawyer in the city.
Wewe ukilipa Fundika kwa Irene Mbowe elfu 20 yeye anakuambia who is Irene Mbowe. Anajua nini?hakuna mtu atakufundisha kuhusu ndoa yako... mnanielewa?
Ila Bible says we perish because of luck of knowledge..(English nimepatia eee..... hahahaha). sasa sijui knowledge inakuja kama mvua ama kwa kujifunza... pyeeeee...
Mnanielewa?
Ukikaa na kutafakari vyema...
Mungu alimuumba Adam kwa ustadi wooote. Kabisaaa.
Kisha akasema si vyema awepeke yake.. haijalishi ustadi ila si vyema awe peke yake.
Mke unaolewa ili ukakamilishe hiyo si vyema.
So cha kufanya ni kuhakikisha unaolewa na real man.
Utaniuliza who is real man then.....
Nakuja............
Loading...