Hatari: Aina 10 za Wanawake Ambao Mwanaume Hafai Kuwa na Uhusiano Nao Zaidi ya Kujitakia Matatizo.
Japo kila mtu anakasoro zake ila kuna tabia ndogo ndogo ambazo huleta maharibiko kwenye mahusiano na kuufanya uhusiano kubadilika kutoka kwenye amani na utamu unaopaswa kuwa nao na kuwa mchungu iwapo mwanaume asipokuwa makini wakati wa uchaguzi wa mwenzi anaetaka kuwa nae.
Kiumeni.com tumejaribu kufanya utafiti na kuongea na wanaume walioachana na wenzi wao pamoja na wale waliopigwa chini japo wanang'ang'ania wao ndo waliowatema wapenzi wao na kuongea nao kwa mapana juu ya nini kiliwafanya wafikia uwamuzi huo mzito wa kuachana na wenzi wao, ndipo tukapata maelezo mengi na kukuandalia wewe mpenzi msomaji wa kiumeni.com aina ya wanawake kumi ambao inakubidi kufikilia mara mbili kwa marefu na mapana kabla ya uwamuzi wa kuamua kumpa sehemu ya maisha yako.
1. Mwanamke Mchungu: Unamjua yule mwanamke ambaye huwa na hasira na jinsia ya kiume muda wote? Huwa haishi kulalamika wanaume huwa ni wapumbavu, mwanaume haaminiki ni kama mbwa, yeye hasira yake huwa ipo juu ya wanaume muda wote na anaona mwanaume hawafai na hawana umuhimu wowote, hii inawezeka inatokea labda sababu ya katendwa na kuvunjwa moyo mara nyingi, mwanamke wa aina hii iwapo akiwekwa ndani huwa ni vurugu, kukosea inatokea ila kwake itakuwa ni matusi na kosa moja dogo atalichukulia kwa uzito wa ajabu ambao hata haupo, akiwa na hasira ni kutukana na kutoa maneno ya chuki na kashifa kutokana na kutendwa kwake nyuma na wanaume na mrundikano wa hisia ambazo hajazitatua moyoni mwake na hasira zake huwa ni za karibu maana anakuwa hamuamini mwanaume wake hivyo yupo tayari tayari kuangalia kosa ili apate sababu.
2. Mwanamke Mchoyo: Ukiwa unahitaji nyumba iwe na furaha na mwenza ambaye anahitaji furaha yako na ya kwake pia, unahitajika sana kukaa mbali na mwanamke mchoyo, mwanamke wa namna hii yeye huwa anakuwa anajiweka mbele tu kuangalia masilahi yake bila kuangalia hisia zako na tofauti na hapo hata ndugu zako wakija sababu ya ile choyo anasababisha mvurugano wa familia na siku zote huwezi kujikuta na furaha zaidi ya kuwaza kutatua tatizo hili kabla hujalimaliza limeingia jingine.
3. Mwanamke Mpenda vitu: mwanamke huyu la kwake pesa, hajakiona hiki anakitaka, kile nacho anataka bila kuangalia hali ya kiuchumi imekaaje, kamuona jirani Mama Naniii kavaa vile na yeye anataka ashindane nae, anakuwa anajari zaidi vitu vya kidunia bila kuangalia familia yake ipo katika hali gani, yupo radhi kuvunja familia, kuvunja uaminifu wake kwako na hata ule wa kidini ili tu hali ya kile anachokuwa anakihitaji moyoni kitimie. Na siku zote huwa hawezi kuwa mwenza mzuri zaidi ya kukuumiza kichwa na kupasua nyongo yako kwa mawazo ya kumridhisha pale ambapo hauna uwezo napo.
4. Mwanamke Mtongozwaji: Umevutika na yule mwanamke ambae yeye huwa na ukaribu na wanaume mmoja au mwingine kupitiliza? Anacheka cheka na mwanaume huyu na yule kama lile limjusi la kwenye mawe linahama kutoka jiwe moja kwenda jingine likitikisa kichwa kwa kujikubali bila kujishitukia na kufanya wanaume wengi wajihisi labda wanapendwa na msichana wako. Inakubidi uwe mwangalifu maana mwanamke wa hivi huwezi kumfanya mwenza wako maana iwapo hata ukimuoa tabia za namna hii huwa ni ngumu kuziondoa na atakuhisi labda unawivu unamfatilia sana sababu ameisha kaa sana nje ya msitari mpaka hajui mwisho wa mipaka ni wapi. Ukimuoa mwanamke huyu usije shangaa kusikia mkeo anasifa ya kujichekelesha kwa wanaume wa mtaa wako.
5. Mama Shughuli: Huyu ni shida, kila aina ya sherehe yeye kaalikwa na zote anaziudhuria, Diamond anaimba kwenye klabu ya karibu saa nane usiku yeye yupo, siku zote yeye anavaa nguo ya fasheni ya kisasa zaidi na ndo mkufunzi wa sherehe zijitokezazo, maisha yake yalishazoea hivyo na furaha yake na maongezi yake yanategemea hafla kubwa ijayo. Mwanamke wa sampuli hii huwa huwezi kumfanya mwenza na kuhisi utajenga nae familia, labda wewe ndo uwe mtunzaji watoto na mchunga nyumba wakati yeye yupo bize usiku na masherehe.
6. Mpenda kupewa kipaumbele: Japo ni jambo la kike kutaka kupewa kipaumbele na jamii, ila ukiwa ni ugonjwa hapa lazima jasho liwe linakutoka kila siku, mwanaume mzuri ni yule anaemjali mkewe, ila kama mke yeye ndo anataka umjali yeye tu, kila ukitaka utoke anataka akuone, hujaenda kibanda cha kuangalia mpira jirani ameshapiga simu urudi anashida na wewe, yeye anataka ya kwake tu bila kuangalia hata wewe unahitaji muda wako binafsi wa mambo mengine, ukiwa na mwenza wa namna hii unakuwa mtuma kwake badala ya kufurahia nawe maisha yako jinsi unavyozeeka polepole, kuishi kwako inakuwa ili umtimizie shida zake yeye.
7. Mwanamke Mbea: Je Saa zote yeye hana ya kwake, anataka kujua flani anaishije na anafanya nini?, mwanamke wa namna hii haumuhitaji. Manaume huitaji mwanamke ambae anauwezo wa kujenga familia na hii inaitaji akili ambayo inauezo a kutatua matatizo yanayoizunguka familia yake, kama mwanamke akili yake ipo bize kuaza Mama Majuto nyumba ya pili leo wamekula nini haezi kua na akili ya kujenga zaidi ya kuongeza umasikini ka kutumia muda wake kusema na kuongelea juu ya wengine badala ya kufanya kazi za kimaendeleo, na utakuwa na wakati mgumu pia wa kumfanya akufikilie kuhusu wewe, unafika nyumbani yeye yuko mtaa wa pili kaendea umbea.
8. Mwanamke Mwenye Deko: Kuna wanawake wengine wameshazoea kudekezwa kwao, na hana tabia ya kufanya kazi ili aweze kujitimizia mahitaji maana hajakuzwa hivyo na hii siku zote haipo kwenye sifa ya mwanamke mzuri na mke mzuri, hata kama ukijitoa na kujitahidi kumpa maisha aliyokwisha zoea, jua kabisa ukimuoa watoto lazima watatokea kwenye familia, na mama mwenye deko hawezi kukuza watoto maana watoto wanahitaji kazi kubwa ya kuwaangalia na kuwakuza. Hivyo mwanamke wa namna hii hatoweza kuwa mwenza mzuri.
9. Mwanamke Ambaye Hana Msimamo: Mwanamke ambae huwa na hali ngumu kufanya maamuzi ya chochote, (kikazi, kijamii, kirafiki, kimahusiano au kwa vyovyote vile..) na hivyo hivyo hatokuwa na uwezo kwenye maamuzi hasa kwenye ndoa, maana atakuwa bendela kifata upepo, mtu akimwambia hiki yeye atakiamini, kile vile vile atafuata huko huko, na itakuwa ngumu pia kuwa mke mzuri maana dunia imejaa maneno mengi na vishawishi vingi.
10. Mwanamke Mwenye Mdomo Mchafu: Je ukigombana naye kidogo maneno yake yanakuwaje? maneno ya kebehi hayamuhishi, akikasirika hata heshima baina yenu inakuwa haipo tena?, vipi kuhusu watu wengine anaowaona wapo chini ya hadhi yake?, Kama majibu unayojijibu yanaelekea hana heshima kwa binadamu wenzake basi hapo umekanyaga bomu, litalipuka muda wowote na iwapo likilipuka lazima litakuumiza kihisia, na iwapo ukimfanya akawa mkeo basi kaka lazima kila jioni baada ya kazi utapitia baa ilio kalibu nawe. Na kiumeni.com inaendelea kukupa pole kwa kuyapa shida maisha yako ambayo yangekuwa matamu zaidi iwapo ungegunduwa