matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Feb 14, 2017

YESU ASIFIWE KWA HILI LA MORAVIAN CHURCH OF TANZANIA

Hatimaye mgogoro uliodumu ndani ya kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Mashariki kwa zaidi ya miaka mitano umeweza kutatuliwa.
Hatimaye mgogoro uliodumu ndani ya kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Mashariki kwa zaidi ya miaka mitano umeweza kutatuliwa na kufikia mwisho, licha ya kusababisha madhara makubwa ndani ya kanisa hilo na kuumiza wengi kiroho.
Akitoa tamko mbele ya kusanyiko la waumini wa kanisa hilo kutoka maeneo mbalimbali na walioonekana kufurahia hatua hiyo, askofu mkuu wa kanisa la Moravian Tanzania, KENAN PANJA, amesema mpasuko huo ulikuwa kama ajali, na wengi wasingependa kuona tatizo hilo likiendelea ndani ya kanisa, hivyo ofisi yake kipindi chote cha mgogoro imekuwa ikiwasiliana na upande wa pili kuona namna gani wanaweza kulirejesha kanisa pamoja kwa nia moja, kanisa la undugu Tanzania na duniani pote.
Nalo jopo la maaskofu wengine wa kanisa hilo pamoja na waumini wameitaka jumuiya ya Moravian kutochanganya imani ya kikristo na siasa, maana sehemu zilizo nyingi ama wanasiasa au siasa zenyewe kanisani, zimekuwa zikiyachanganya makanisa, hivyo wajitahidi kuwa mbele za Mungu.
Mgogoro ndani ya kanisa la Moravian jimbo la Mashariki, Dar es salaam, limekuwa na mpasuko ulioanza mwaka 2013 baaada ya sinodi kuchagua halmashauri kuu ya jimbo inayoongozwa sasa na mwenyekiti Mchungaji SAMWEL YESAYA MWAISEJE, ambapo wale ambao hawakufika kwenye sinodi hiyo waliona kwanini waliachwa nje na wao wakaanza kutafuta halmashauri yao na nafasi ya kuwa na jimbo lao.
Hatua ambayo ilishindikana kufuatia utaratibu wa kanisa hilo duniani, jimbo hupatikana na halmashauri kuu ya kanisa la Moravian duniani na hiyo ndio iliyokubali lianzishwe jimbo la Mashariki na hivyo kutambua uhalali wa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...