matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Apr 18, 2012

TANGAZO KWA WAANDAAJI NA WAMILIKI WA GOSPEL BLOGS NA WOTE WANAOPENDA KUANZISHA BLOG ZA KIKRISTO

Tarehe 21 April 2012 kuanzia saa 3:00 Asubuhi mpaka saa 5:00 Asubuhi katika mgahawa wa Maarufu wa
Bulls(Esarp Village) Ulioko maeneo ya Survey pembeni ya Mlimani City.Kutafanyika mkutano maalumu utakaowakutanisha wamiliki wa blogs za kikristo nchini walio ndani na nje ya Dar es salaam. Sambamba na hilo pia itakuwa ni fursa kwa watumishi wote ambao kwa namna moja au nyingine wana nia kuanzisha blog kwa ajili ya huduma na taasisi zao,makanisa yao, pamoja na vikundi vya injili vilivyoko mashuleni,na vyuoni.

Lengo kubwa la mkutano huu ni;

1.Kufahamiana

2.kusaidiana kiufundi namna ya kuboresha na ku-run Blog

3.Kuelimishana na kukumbushana misingi ya uandishi hususani huu wa kutumia blogs na mitandao ya jamii(Citizen Journalism).

Blog kama MADHABAHU, ikitumiwa Vizuri inaweza kumtukuza Mungu na ikitumiwa ndivyo sivyo inaweza
kulitukanisha jina la Kristo.Ule mzigo wa Ki-Mungu, ambao Mungu ameuweka ndani ya wamiliki wa blogs na
wote wenye nia ya kufungua blog ni HESHIMA kubwa.Hivyo namna ya kutembea na Heshima hiyo inamuhitaji

Mungu na kukumbushana pamoja na kusaidiana kwa Upendo.Tafadhali fika Bila kukosa kwa kwa lengo la kuujenga ufalme wa Mungu.


Tunatambua kuna bloggers wengi wako nje ya Nchi na Wako Nje ya Dar, tumetengeneza Christian Bloggers Forum kwenye Facebook, itaanza kuwa Active Kuanzia Leo Baadae na baada ya hapo tutakuwa tunapeana Update za Kila Siku kupitia Forum.

KIBWAGIZO: Kwa Watakaokuja Njoo na Sh 2000 kwa ajili ya Chai Yako Mwenyewe Utakayojinunulia, hakuna Kiingilio.


Hakuna Kiingilio.

Kwa Mawasiliano Zaidi


Coordinators.

0713 494110

0713-763939
SOURCE; http://samsasali.blogspot.com/

LISTI YA BAADHI YA BLOG ZA INJILI TANZANIA
*http://iyeleleteam.blogspot.com/
*http://hosannainc.blogspot.com/
*http://mabisatz.blogspot.com/
*http://unclejimmytemu.blogspot.com/
*http://www.gospelkitaa.blogspot.com/
*http://samsasali.blogspot.com/
*http://www.nyimbozadini.blogspot.com/
*johnshabani.blogspot.com
* strictlygospel.wordpress.com/
* kabulageorge.blogspot.com/
* http://2gkitangalagospels.blogspot.com/
*http://sayuni.blogspot.com/
*http://sanga.wordpress.com/
*http://www.kaysontz.blogspot.com/

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...