matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

May 28, 2012

ZANZIBAR IMEGEUKA UWANJA WA VITA GHAFLA. Yajitia doa baada ya kusafika kwa mwaka mmoja wa maridhiano


 Mmoja wa waandamani wa Kundi la Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) Kisiwani Unguja,Zanzibar akionyeshan kitambaa kilicho na Damu mapema leo Asubuhi wakati wakiendelea na maandamano yao ambayo yamesababisha vurugu kubwa kisiwani humO



 Zanzibar yajitia doa baada ya kusafika kwa mwaka mmoja wa maridhiano
Barabara ya michenzani ikiwa tuli hali kama mnavyoiona hapa

 Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine. Vijana baada ya kutembea wakionesha ujumbe wao kwa waandishi wa habari


 Jeshi la polisi likizunguka zunguka maeneo ya mijini ambapo muda mfupi tu mabomu matatu yamerushwa eneo la michenzani na darajani na watu kadhaa kukimbi

 KABLA:
Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine. Mmewaona akina mama eeeh wapo mbele kwa hivyo kama ni kutokea khatari basi wangeanzwa wao,


BAADA:
 Hali imerejea upya kama juzi na jana katika maeneo ya mani ambapo mamia ya waandamanaji wanapigwa mabomu ya machozi hivi sasa inshallah salama na mani itarejea lakini hali sio nzuri kwa hakika

 Kikao cha pamoja kati ya waziri wa mambo ya ndani Tanzania, Emmanuel Nchimbi, mkuu wa jeshi la polisi Said Ali Mwema, viongozi wa taasisi za kiislamu, maafisa wa serikali, ZATI, na maafisa wa ubalozi waliohakikisha kurejesha hali ya usalama Zanzibar bado hakijazaa matunda baada ya matukio waliokubaliana kusitishwa kuendelea jioni hii ya leo katika maeneo ya Amani, Darajabovu, Mwanakwerekwe na Mpendae




 Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) liliopo eneo la Kariakoo lachomwa moto jana usiku

 Vifaa na vya kanisa la vimechomwa moto usiku wa jana ikiwemo viti na vitu vyengine ambapo thamani yake pamoja na gari ni shilingi millioni 120 kwa mujibu wa Bishop Dickson Maganga wa kanisa hilo


  moto uliowanshwa na vijana wakisema wataendelea kudai haki zao katika maeneo ya michenzani kuelekea mlandege
KABLA:  Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine. Akina mama wao walikuwa mstari wa mbele
 

KABLA:  Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine. Baada ya kurudi katika matembezi au ukipenda utaita maandamano ya amani au maandamano ya ghafla



GARI LA MCHUNGAJI MASKINI WE LILICHOMWA MOTO KWENYE TUKIO HILI........

MWSHO HAPO JANA;

Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa anasema hivi. "Tutaendelea kuwasaka Viongozi wa Uamsho kwa gharama zote"

SOURCE:  http://www.facebook.com/profile.php?id=721596175

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...