PICHA NA BAADHI YA MATUKIO KATIKA SIKU YA UZINDUZI PALE CCC UPANGA DAR ES SALAAM.
Wanakamati walioandaa shughuli nzima wanatambulishwa ukumbini ccc upanga
DFD
Wanakamati wakiwa kwenye jukwaa
kwaya ya Magomeni vijana AICT wakifanya mashambulizi kwa shetani na nyimbo yao mpya ya Thamani yangu kwa Bwana naijua. hawa ni vijana tupu hakuna mzee hapa ni kazi mbele kwa mbele.
kwaya ya AICT magomeni hawakukosa. waliiimba vizuri. hii ni kwaya kongwe sana ambayo ndani yake ina wakina dada ma solo wazoefu mmojawapo akiitwa Mercy Nyagaswa ambaye alishawahi kutoa album yake binafsi miaka ya nyuma.
hapa mwanamuziki wa nyimbo za injili akimpa Mungu utukufu
Wazazi wa Josephine Minza wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa binti yao. Matunda ya malezi bora ni chanzo cha haya yote.
Vijana hatari sana hawa wakipiga sebene moja matata mno stegini. walianza kama vile taratibu ila baadae ukumbi wote ulisimama.
CCC upanda watu walikuwa wengi siku hiyo
Sebene ikipigwa
Mungu akimtumia kijana wake katika nyimbo yake nzuri inayoitwa Ni kwa neema tu. Jina lake kijana huyu machachari ni Mwaisabite Edson
MINZA JUKWAANI AKIWAKILISHA
hapa tunaona collaboration kati ya minza na back vocalist wake
Mgeni Rasmi akizindua album hapa pembeni kushoto ni Mwalimu wa minza anayempa mawazo na theme ya DVD yake ya maisha ya ibada ambaye ndiye alitoa neno siku hiyo. wakati kulia ni wazazi wa minza.
MAISHA YA IBADA