Ni kawaida nchini Kenya, hasa Nairobi, kukaguliwa wakati
wa kuingia kwenye maduka makubwa ya maeneo mengine yenye mikusanyiko,
lakini safari hii ukaguzi huo haukusaidia
JENGO LA WESTGATE LIKIFUKA MOSHI BAADA YA ASKARI NA VIKOSI KUPAMBANA NA MAGAIDI NDANI YA JENGO SIKU CHACHE ZILIZOPITA.
JUU: WATU WAKIOKOLEWA KUTOKA NDANI YA JENGO HILO LA WESTGATE
Jumamosi Septemba 21 ilikuwa siku ya kawaida kwa
Wakenya wa matabaka mbalimbali. Wengi walibaki majumbani wakipumzika
baada ya juma zima la kukurukakara za kutafuta riziki. Kwa wengine
ilikuwa siku ya ujenzi wa taifa na walikwenda kazini kama kawaida.
Wengine waliamua kwenda kujivinjari katika sehemu mbalimbali za kujiburudisha. Hali haikuwa tofauti kwa wakazi wa eneo la Westlands ambalo ni sehemu inayohusishwa na walala hai.
West Gate, kwa miaka mingi, imekuwa mahali pa
mabwenyenye na wageni kutoka nje wanaofanya kazi katika mashirika
makubwa makubwa kama vile Umoja wa Mataifa hujiburudisha huku wakinunua
wanachotaka. Ina maduka mengi makubwa pia imejengwa katikati ya mitaa ya
kifahari.
Siku hiyo, muda wa saa sita na nusu mchana Kituo
cha Televisheni cha Nation (NTV) kilitangaza kwamba kumekuwa na tukio
la uhalifu West Gate. Kadiri saa ziliposonga ndipo ikadhihirika kwamba
kumbe si wizi bali shambulizi la kigaidi.
Kuanzia hapo, tukio hilo likaanza kuvutia vituo
vingine vya habari vilivyofunga virago vyao kuelekea huko ili
vipeperushe habari za moja kwa moja kutoka eneo la tukio.
Kisa hiki ambacho sasa kimewaua takriban watu 62 kimeshangaza dunia na kuvishtukiza vikosi vya ulinzi vya Kenya.
Wavamizi wamejitambulisha katika mitandao ya
kijamii kama vile Twitter kuwa ni waasi wa kundi haramu la Al-Shabaab na
wanalipiza kisasi cha uvamizi wa majeshi ya Kenya Somalia. Kituo cha
Televisheni cha Al-Jazeera kilikuwa kituo cha kwanza cha habari
kutangaza kwamba waliofanya uvamizi huo ni Al-Shabaab.
Baada ya saa 24 na nne tangu uvamizi huo ufanyike,
vikozi vya ulinzi vya Kenya (KDF) vilivamia jengo hilo Jumapili na
wakawaokoa mateka wengi. Hata hivyo, bado kulikuwa kuna watu wazima na
watoto waliokuwa ndani wakihangaishwa na watekaji nyara hao wapatao 15.
Walioshuhudia kisa hicho wanasema kwamba, wavamizi
waliingia jengo hilo baada ya kurusha maguruneti na kuwamiminia risasi
walinzi na watu waliokuwa wakinunua bidhaa.
Baadhi ya viongozi waliowasili katika eneo hilo
kujionea yaliyokuwa yakiendelea, ni aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga
na Seneta Moses Wetangula. Viongozi hao walihutubia taifa wakisema
kwamba tukio hilo limewaleta pamoja Wakenya bila kujali misingi ya
kikabila au rangi.
KDF walipoingia jengo hilo, walifanikiwa kushika
doria katika maeneo mbalimbali ambapo yaliweza kupata fursa nzuri ya
kukabiliana na adui. Vikosi hivyo vilishirikiana na FBI ya Marekani,
Mosad ya Israel na M16 ya Uingereza katika harakati hizo.
Baada ya mashambulio ya kigaidi kwenye mall ya Westgate huko Nairobi,
Peter Msechu amekuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kutoa wimbo
maalum kwa ajili ya tukio hilo. Peter Msechu anasema kwamba kwa kutambua
mchango watu wa Kenya kwenye muziki wake. Ameamua kutoa wimbo huu
maalum kwa kuwafuta machozi wananchi wa taifa la Kenya.Sikila na
download hapa