Prime Minister: "Aisee jana na leo jasho limenitoka, yani wewe mwanangu zitto unataka kunitoa nishai mbele ya umma mh"
Zitto: "Hapana hapana mzee sio hivyo mkuu. Unajua wakati mwingine kukumbushana ni muhimu sana kwani bila hivyo hao watendaji wasingejikosoa. nafikiri nime play part yangu vizuri"
Hamad: "Tehe tehe tehe mimi sina la kusema Mkuu si unakumbuka hata mimi niling'olewa ila nikanusurika tu. ni ubishi tu hapa. ila mzee tupo pamoja katika hili"
Mnyika: "hata leo nilipokuwa nasema jambo dogo tu la kurekebisha kipengele aisee nilishambuliwa mh we acha tu zitto. eti jamaa wanataka gati fasta fasta hivi wanadhani hii mikopo ya china ina riba ndogo. ni zaidi ya asilimia 70 sasa hii tutakuwa tunajenga ama tunabomoa. bora tuchelewe tufike. Mkuu si unajua ule msemo kawia ufike"
Prime Minister: "Ninyi vijana kweli mmefanya niamke. kweli ninazeeka tu huu mwili ila naamini maini hayazeeki. Sitawaangusha tena tuvumiliane ni mapito tu haya. yatapita..............."
Hata hivyo blog hii imemsikia Zitto akisema yeye hana uhakika kama maamuzi ya wana CCM ni kuwaengua mawaziri ama la. na pia ikumbukwe leo mheshimiwa waziri mkuu akitoka bungeni alisema kuwa hayuko tayari kuzungumza chochote hadi siku ya jumatatu ambapo bunge la jamuhuri litahairishwa hadi kikao kijacho.
Tunasubiri jumatatu tuone yatakayojiri..........................
Endapo watajiuzulu mawaziri kadhaa basi yafuatayo ni baadhi ya magazeti yakionyesha utabiri wao..
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge, John Mnyika wa Ubungo (kushoto), Kabwe Zitto wa Kigoma Kaskazini na Hamad Rashid wa Wawi, kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 21, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)