matukio burudani injili uimbaji maisha sanaa muziki maigizo habari maajabu vichekesho maendeleo mafanikio uchumi lugha maono mahubiri nyimbo biblia siasa

Feb 20, 2018

Jan 20, 2018

Emmanuel Mbasha stejini

Anaendelea vyema. Utukufu kwa Mungu

Oct 22, 2017

God is still Good

God is wonderful. Try him

Feb 28, 2017

UZINDUZI WA BETTY BARONGO ULIVYOFANA MAKAMBAKO UKISINDIKIZWA NA BEATRICE KITAULI.

"Huu ndio uzinduzi wa Betty Barongo wa kihistoria uliofanyika Makambako Yeriko mpya EAGT jumapili hii.. Beatrice kitauli muimbaji kutoka morogoro ndiye alikuwa Mgeni aliyealikwa wa shughuli katika uimbaji kumsindikiza huyu mwanamuziki chipukizi aliandika haya kwenye page yake ya facebook akasema "Siku ikaisha na tukaendelea kumnywa roho mtakatifu kwa mguso wa kipekee. Na watu wa makambako wakatusapoti sana kwa kujumuika na sisi kumtukuza Mungu wa mbinguni. Asanteni sana watu wa Mungu.... Tukutane Arushaaa mwezi Mach 2017"

HAPA NI MATUKIO KATIKA PICHA JINSI ILIVYOKUWA. Watu WALIFURIKA.

Feb 17, 2017

ATOSHA KISSAVA


"Maana ninayajua Mawazo niwawaziayo ninyi...asema Bwana, SI MABAYA,ni mawazo ya AMANI,kuwapa Tumaini siku zenu zote"! Mungu anatuwazia mema sikuzote rafiki yangu USIYUMBISHWE NA CHOCHOTE..MTAZAME YEYE  SIKUZOTE,KATIKA HALI YOYOTE,WAKATI WOWOTE,UTAKUWASALAMA.

Feb 15, 2017

USIICHUKULIE SIMPLE ITAKUCOST. SOMA HII WEWE UNAYETAKA KUOA

Hatari: Aina 10 za Wanawake Ambao Mwanaume Hafai Kuwa na Uhusiano Nao Zaidi ya Kujitakia Matatizo.
Japo kila mtu anakasoro zake ila kuna tabia ndogo ndogo ambazo huleta maharibiko kwenye mahusiano na kuufanya uhusiano kubadilika kutoka kwenye amani na utamu unaopaswa kuwa nao na kuwa mchungu iwapo mwanaume asipokuwa makini wakati wa uchaguzi wa mwenzi anaetaka kuwa nae.
Kiumeni.com tumejaribu kufanya utafiti na kuongea na wanaume walioachana na wenzi wao pamoja na wale waliopigwa chini japo wanang'ang'ania wao ndo waliowatema wapenzi wao na kuongea nao kwa mapana juu ya nini kiliwafanya wafikia uwamuzi huo mzito wa kuachana na wenzi wao, ndipo tukapata maelezo mengi na kukuandalia wewe mpenzi msomaji wa kiumeni.com aina ya wanawake kumi ambao inakubidi kufikilia mara mbili kwa marefu na mapana kabla ya uwamuzi wa kuamua kumpa sehemu ya maisha yako.

1. Mwanamke Mchungu: Unamjua yule mwanamke ambaye huwa na hasira na jinsia ya kiume muda wote? Huwa haishi kulalamika wanaume huwa ni wapumbavu, mwanaume haaminiki ni kama mbwa, yeye hasira yake huwa ipo juu ya wanaume muda wote na anaona mwanaume hawafai na hawana umuhimu wowote, hii inawezeka inatokea labda sababu ya katendwa na kuvunjwa moyo mara nyingi, mwanamke wa aina hii iwapo akiwekwa ndani huwa ni vurugu, kukosea inatokea ila kwake itakuwa ni matusi na kosa moja dogo atalichukulia kwa uzito wa ajabu ambao hata haupo, akiwa na hasira ni kutukana na kutoa maneno ya chuki na kashifa kutokana na kutendwa kwake nyuma na wanaume na mrundikano wa hisia ambazo hajazitatua moyoni mwake na hasira zake huwa ni za karibu maana anakuwa hamuamini mwanaume wake hivyo yupo tayari tayari kuangalia kosa ili apate sababu.

2. Mwanamke Mchoyo: Ukiwa unahitaji nyumba iwe na furaha na mwenza ambaye anahitaji furaha yako na ya kwake pia, unahitajika sana kukaa mbali na mwanamke mchoyo, mwanamke wa namna hii yeye huwa anakuwa anajiweka mbele tu kuangalia masilahi yake bila kuangalia hisia zako na tofauti na hapo hata ndugu zako wakija sababu ya ile choyo anasababisha mvurugano wa familia na siku zote huwezi kujikuta na furaha zaidi ya kuwaza kutatua tatizo hili kabla hujalimaliza limeingia jingine.

3. Mwanamke Mpenda vitu: mwanamke huyu la kwake pesa, hajakiona hiki anakitaka, kile nacho anataka bila kuangalia hali ya kiuchumi imekaaje, kamuona jirani Mama Naniii kavaa vile na yeye anataka ashindane nae, anakuwa anajari zaidi vitu vya kidunia bila kuangalia familia yake ipo katika hali gani, yupo radhi kuvunja familia, kuvunja uaminifu wake kwako na hata ule wa kidini ili tu hali ya kile anachokuwa anakihitaji moyoni kitimie. Na siku zote huwa hawezi kuwa mwenza mzuri zaidi ya kukuumiza kichwa na kupasua nyongo yako kwa mawazo ya kumridhisha pale ambapo hauna uwezo napo.

4. Mwanamke Mtongozwaji: Umevutika na yule mwanamke ambae yeye huwa na ukaribu na wanaume mmoja au mwingine kupitiliza? Anacheka cheka na mwanaume huyu na yule kama lile limjusi la kwenye mawe linahama kutoka jiwe moja kwenda jingine likitikisa kichwa kwa kujikubali bila kujishitukia na kufanya wanaume wengi wajihisi labda wanapendwa na msichana wako. Inakubidi uwe mwangalifu maana mwanamke wa hivi huwezi kumfanya mwenza wako maana iwapo hata ukimuoa tabia za namna hii huwa ni ngumu kuziondoa na atakuhisi labda unawivu unamfatilia sana sababu ameisha kaa sana nje ya msitari mpaka hajui mwisho wa mipaka ni wapi. Ukimuoa mwanamke huyu usije shangaa kusikia mkeo anasifa ya kujichekelesha kwa wanaume wa mtaa wako.

5. Mama Shughuli: Huyu ni shida, kila aina ya sherehe yeye kaalikwa na zote anaziudhuria, Diamond anaimba kwenye klabu ya karibu saa nane usiku yeye yupo, siku zote yeye anavaa nguo ya fasheni ya kisasa zaidi na ndo mkufunzi wa sherehe zijitokezazo, maisha yake yalishazoea hivyo na furaha yake na maongezi yake yanategemea hafla kubwa ijayo. Mwanamke wa sampuli hii huwa huwezi kumfanya mwenza na kuhisi utajenga nae familia, labda wewe ndo uwe mtunzaji watoto na mchunga nyumba wakati yeye yupo bize usiku na masherehe.

6. Mpenda kupewa kipaumbele: Japo ni jambo la kike kutaka kupewa kipaumbele na jamii, ila ukiwa ni ugonjwa hapa lazima jasho liwe linakutoka kila siku, mwanaume mzuri ni yule anaemjali mkewe, ila kama mke yeye ndo anataka umjali yeye tu, kila ukitaka utoke anataka akuone, hujaenda kibanda cha kuangalia mpira jirani ameshapiga simu urudi anashida na wewe, yeye anataka ya kwake tu bila kuangalia hata wewe unahitaji muda wako binafsi wa mambo mengine, ukiwa na mwenza wa namna hii unakuwa mtuma kwake badala ya kufurahia nawe maisha yako jinsi unavyozeeka polepole, kuishi kwako inakuwa ili umtimizie shida zake yeye.

7. Mwanamke Mbea: Je Saa zote yeye hana ya kwake, anataka kujua flani anaishije na anafanya nini?, mwanamke wa namna hii haumuhitaji. Manaume huitaji mwanamke ambae anauwezo wa kujenga familia na hii inaitaji akili ambayo inauezo a kutatua matatizo yanayoizunguka familia yake, kama mwanamke akili yake ipo bize kuaza Mama Majuto nyumba ya pili leo wamekula nini haezi kua na akili ya kujenga zaidi ya kuongeza umasikini ka kutumia muda wake kusema na kuongelea juu ya wengine badala ya kufanya kazi za kimaendeleo, na utakuwa na wakati mgumu pia wa kumfanya akufikilie kuhusu wewe, unafika nyumbani yeye yuko mtaa wa pili kaendea umbea.

8. Mwanamke Mwenye Deko: Kuna wanawake wengine wameshazoea kudekezwa kwao, na hana tabia ya kufanya kazi ili aweze kujitimizia mahitaji maana hajakuzwa hivyo na hii siku zote haipo kwenye sifa ya mwanamke mzuri na mke mzuri, hata kama ukijitoa na kujitahidi kumpa maisha aliyokwisha zoea, jua kabisa ukimuoa watoto lazima watatokea kwenye familia, na mama mwenye deko hawezi kukuza watoto maana watoto wanahitaji kazi kubwa ya kuwaangalia na kuwakuza. Hivyo mwanamke wa namna hii hatoweza kuwa mwenza mzuri.

9. Mwanamke Ambaye Hana Msimamo: Mwanamke ambae huwa na hali ngumu kufanya maamuzi ya chochote, (kikazi, kijamii, kirafiki, kimahusiano au kwa vyovyote vile..) na hivyo hivyo hatokuwa na uwezo kwenye maamuzi hasa kwenye ndoa, maana atakuwa bendela kifata upepo, mtu akimwambia hiki yeye atakiamini, kile vile vile atafuata huko huko, na itakuwa ngumu pia kuwa mke mzuri maana dunia imejaa maneno mengi na vishawishi vingi.

10. Mwanamke Mwenye Mdomo Mchafu: Je ukigombana naye kidogo maneno yake yanakuwaje? maneno ya kebehi hayamuhishi, akikasirika hata heshima baina yenu inakuwa haipo tena?, vipi kuhusu watu wengine anaowaona wapo chini ya hadhi yake?, Kama majibu unayojijibu yanaelekea hana heshima kwa binadamu wenzake basi hapo umekanyaga bomu, litalipuka muda wowote na iwapo likilipuka lazima litakuumiza kihisia, na iwapo ukimfanya akawa mkeo basi kaka lazima kila jioni baada ya kazi utapitia baa ilio kalibu nawe. Na kiumeni.com inaendelea kukupa pole kwa kuyapa shida maisha yako ambayo yangekuwa matamu zaidi iwapo ungegunduwa

Feb 14, 2017

RATIBA YA JOHN LISU MARCH 2017

JOHN LISU:
Watu wa Mungu wa Arusha Nitakuwepo Arusha wiki ya tarehe 1/3/2017 hadi Tarehe 5/3/2017 Kama ungependa nije Kwenye Kikundi chako au Timu ya kusifu Na Kuabudu au ungependa nitembelee Team yako au Yenu Ili kuongea Na kubadilishana mawazo katika huduma tuliyo nayo,waweza kuni Inbox.

YESU ASIFIWE KWA HILI LA MORAVIAN CHURCH OF TANZANIA

Hatimaye mgogoro uliodumu ndani ya kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Mashariki kwa zaidi ya miaka mitano umeweza kutatuliwa.
Hatimaye mgogoro uliodumu ndani ya kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Mashariki kwa zaidi ya miaka mitano umeweza kutatuliwa na kufikia mwisho, licha ya kusababisha madhara makubwa ndani ya kanisa hilo na kuumiza wengi kiroho.
Akitoa tamko mbele ya kusanyiko la waumini wa kanisa hilo kutoka maeneo mbalimbali na walioonekana kufurahia hatua hiyo, askofu mkuu wa kanisa la Moravian Tanzania, KENAN PANJA, amesema mpasuko huo ulikuwa kama ajali, na wengi wasingependa kuona tatizo hilo likiendelea ndani ya kanisa, hivyo ofisi yake kipindi chote cha mgogoro imekuwa ikiwasiliana na upande wa pili kuona namna gani wanaweza kulirejesha kanisa pamoja kwa nia moja, kanisa la undugu Tanzania na duniani pote.
Nalo jopo la maaskofu wengine wa kanisa hilo pamoja na waumini wameitaka jumuiya ya Moravian kutochanganya imani ya kikristo na siasa, maana sehemu zilizo nyingi ama wanasiasa au siasa zenyewe kanisani, zimekuwa zikiyachanganya makanisa, hivyo wajitahidi kuwa mbele za Mungu.
Mgogoro ndani ya kanisa la Moravian jimbo la Mashariki, Dar es salaam, limekuwa na mpasuko ulioanza mwaka 2013 baaada ya sinodi kuchagua halmashauri kuu ya jimbo inayoongozwa sasa na mwenyekiti Mchungaji SAMWEL YESAYA MWAISEJE, ambapo wale ambao hawakufika kwenye sinodi hiyo waliona kwanini waliachwa nje na wao wakaanza kutafuta halmashauri yao na nafasi ya kuwa na jimbo lao.
Hatua ambayo ilishindikana kufuatia utaratibu wa kanisa hilo duniani, jimbo hupatikana na halmashauri kuu ya kanisa la Moravian duniani na hiyo ndio iliyokubali lianzishwe jimbo la Mashariki na hivyo kutambua uhalali wa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo.

Feb 13, 2017

MUZIKI BILA MADAWA YA KULEVYA INAWEZEKANA-TID

https://youtu.be/O72ws62WgFk

Feb 12, 2017

GWAJIMA ALIPOTOKA KUSHIKILIWA CENTRAL KAANDIKA HAYA KWENYE PAGE.

GWAJIMA ALIPOTOKA ALITOA SHUKRANI HIZI::
"Kesho nitakuwepo kwaajili ya Ibada ya Jumapili, Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar es Salaam.  Mungu awabariki sana nawapenda nawaombea wote mlioomba kwaajili ya Hili. I'm a #Heavenlyman @bishopgwajima @bishopgwajima @bishopgwajima"

Feb 11, 2017

Feb 9, 2017

MZEE WA UPAKO ASEMA TB JOSHUA NI TAPELI.


TB Joshua tapeli - Mzee wa Upako

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama 'Mzee wa Upako' ametema cheche kwa Nabii maarufu kutoka Nigeria TB Josua wa Kanisa la SCOAN kuwa ni tapeli na kusisitiza kuwa hapaswi kuaminiwa kwa lolote.

Akijibu maswali katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Mch. Lusekelo amesema kuwa Nabii TB Joshua ni tapeli kwani alikwisha tabiri uchaguzi wa Marekani kuwa Bi. Hillary Clinton atashinda lakini matokeo yakawa tofauti na utabiri pamoja na uchaguzi wa Tanzania alikosea kutabiri ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.
Aidha Lusekelo amezidi kupigilia msumari huo kwa kudai kuwa TB Joshua hana unabii unaosomwa kwenye biblia kama kina nabii Elisha, Eliya na wengineo ambao walikuwa na uwezo wa kuona vita au maadui kabla hata hawajakaribia katika maeneo ya ufalme.
"Yule ni tapeli kwa sababu nchini kwake kuna wale mabinti waliotekwa kipindi kile mpaka leo ameshindwa kuwakomboa sasa mtu kama huyo unamuamini vipi? si mliona alimtabiria yule mama Hillary atakuwa Rais lakini akakosea hata hapa nchini si alitabiria watu watano watakuwa marais katika hali ya kawaida nchi itaongozwaje na marais wote hao ?" alihoji Mzee wa upako
Lusekelo aliongeza pia kuwa siyo kila mtu anaweza kuwa nabii huku (bila kuziweka hadharani) akisema unabii unahatua zake na sifa zake ambazo TB Joshua hana na ndiyo maana alishindwa hata kuona kuwa jengo la kanisa lake linaelekea kuanguka na badala yake akaacha watu wakapoteza maisha huku yeye akienda Afrika Kusini.
Source: Eatv fb fun page

Feb 6, 2017

NDOA ILIYOKWELI

TUMEPAKUA HII YA NDOA:
HIVI NILISHAFUNDISHA HII?
IRENE MBOWE SAYS:
KESHO NITAKUWA NA SOMO AMBALO NI VERY SENSTIVE. SOMO NYETI SANA.
NIOMBEJE KWA AJILI YA MUME.
ILA ITAKUWA VIZURI KAMA NITAANZA NA SOMO HILI HAPA.
Unatamani Ndoa ama Harusi?
Yaani unataka Mume ama Harusi?
Ndoa ni Mume.
Harusi ni Sherehe.
Si ndio eeee.

Mh...Nikiangalia msichana anavyohangaikia harusi.
Kwanza kabla ya harusi anavyohangaikia uchumba...
Yani mna zile pozi zenu za engagement..
Kijana anapiga magoti anakuvika pete.
Kisha unapiga picha mkono wa pete unasambaza mitandao yoote.
Na maneno THANKS GOD I FOUND HIM. HUBBY TO BE.

Nikifanikiwaga kupna picha hizi huwa nashinda siku nzima kwenye profile ya mdada huyo mwenye hizo picha. Naanza kuangalia profile yake mwanzo mwisho.
Kisha nasema.

MUNGU MPE AKILI NJEMA  HUYU MSICHANA ANAYEINGIA NDOANI.
Isiwe alitaka Harusi badala ya Ndoa.
Maana ni kama namuona atakavyopata kichaa cha Ndoa baada ya muda fulani ambao ni chini ya 5 yrs ndani ya ndoa.

Anayetaka HARUSI mara nyingi...
1. Hajali anaolewa na nani.
2. Hawezi na hayuko tayari kuhudumia Ndoa.
3.Divorce haimsumbui. Anaiishi.

Anayetaka NDOA Mara nyingi....
1.Anajali sana anaolewa na nani.
2.Anaweza na yuko tayari kuhudumia ndoa.
(Mpaka machozi yananilenga lenga)Najua huyu ni Mjeshi. I said. Mjeshi anapambanaga tu nyakati zote.
3.Hataki kusikia kitu kinaitwa Divorce.
MUNGU WASAIDIE WANAWAKE WOOTE WENYE UTAYARI WA NDOA.
                    
                       ***********
                   SEHEMU YA PILI
Matokeo mazuri ya ndoa bora yanategemea sana umeolewa na nani. Na wewe ni nani.
Biblia inasema  Mwanamume atakutawala.
Mume ni mtawala.
Sasa najiuliza haraka tu. Unaingia kwa mtawala wa aina gani.
Maana Mtawala Bora ama kwa hakika Utawala wake unakuwa wa haki. Si ndio?
Ok ok. Juzi kati Mwl Mwakasege  kafundisha habari ya MKUU ASIYE NA AKILI HUTESA WATU.
So Mume ni mkuu wa familia. Anapokuwa hana akili inakuwaje?????anatesa familia si ndio eee.

Ok ok. So unaolewa na nani?ndilo swali la msingi la kujiuliza.
Hapa na deal na wanaotaka Ndoa. Yaani Mume.
Wanaotaka harusi nitawasaidia kuwaambia best mc... best cake maker.. best salon na best mpambaji.
Ila kwa wanaotaka Ndoa naomba hili weka akilini nani anakuoa.
Juzi tumesoma habari ya SEX IS NOT LOVE.
Hii inahusika na mmeshaisoma.

Sasa nani wa kukuoa.  Ndicho kingine.
Nikisoma mahali. Kwa Samuel Nathaniel Sasali. Sijui ni Insta ama hapa face book.
Aliongea vyema.
Kwamba wanandoa wanapoingia ndoani wanajua yanayowakabili?
Nusura nidondoshe chozi.
Nikasoma pale "Mkikosa watoto inakuwaje.. mkipata watoto walemavu inakuwaje.... mmoja akaugua inakuwaje?
NDIO MAANA NATAKA MKE UWE MJESHI. Hivi ndivyo vita vya kupambana navyo mke.
UNATAKA NDOA.
SIO???
Uwe na utayari. Kuhudumia ndoa. Wakati unaofaa na usiofaa.
Uwe tayari kujifunza UPENDO.
Maana unaingia sasa ndoani.
Anaweza kubadilika... ama la anaweza asiwe uliyemtegemea... what next?
Anayeolewa na kuishi Divorce hii haimsumbui kabisa. Its easy.
Wewe ukiuliza watumishi gani wanaweza kunipa msaada wa maombi  yeye anauliza who is the best lawyer in the city.

Wewe ukilipa Fundika kwa Irene Mbowe elfu 20 yeye anakuambia who is Irene Mbowe. Anajua nini?hakuna mtu atakufundisha kuhusu ndoa yako... mnanielewa?
Ila Bible says we perish because of luck of knowledge..(English nimepatia eee..... hahahaha). sasa sijui knowledge inakuja kama mvua ama kwa kujifunza... pyeeeee...
Mnanielewa?

Ukikaa na kutafakari vyema...
Mungu alimuumba Adam kwa ustadi wooote. Kabisaaa.
Kisha akasema si vyema awepeke yake.. haijalishi ustadi ila si vyema awe peke yake.

Mke unaolewa ili ukakamilishe hiyo si vyema.
So cha kufanya ni kuhakikisha unaolewa na real man.
Utaniuliza who is real man then.....
Nakuja............
Loading...

Feb 2, 2017

PUMZIKA KWA AMANI LUNDI TYAMARA GOSPEL MUSICIAN WA AFRICA KUSINI

Johannesburg – South African multi-award winning gospel artist Lundi Tyamara died on Friday at the age of 38 after a battle with stomach TB and a liver condition, his family confirmed.

The Tyamara family released a statement on Friday morning confirming that the musician – who was known for his popular hits including "Mphefumlo Wami" and "Ndixolele" – had passed away just after midnight at the Edenvale Hospital.

Tyamara had been admitted to hospital four weeks ago suffering from abdominal tuberculosis (TB) and a liver condition, his manager Anele Hlazo said.

He took a turn for the worse on Monday and was moved to ICU and put on life support.

"We got the call just after 1am this morning. We are all shocked. We never expected this to happen. The family is taking it very hard."

His death comes a day after a night vigil was held at Central Methodist Church in Johannesburg CBD to pray for his recovery. Condolences for his passing have been pouring in over social media since news broke in the early hours on Friday.

Johannesburg mayor Herman Mashaba tweeted: "Deep condolences to the family of gospel singer and star Lundi Tyamara who passed on earlier. May his soul rest in peace."

Veteran entertainment journalist Lesley Mofokeng said: "He put up a good fight. He ran his race and now belongs to the ages. Rest in perfect peace Lundi Tyamara."

The family was yet to announce plans for a funeral.

Tyamara's death follows that of another gospel legend, Sfiso Ncwane, who died last month aged 37 after a short illness with kidney failure.

WEWE NI Mungu

https://youtu.be/4C7PEiXSId8

Feb 1, 2017

THROW BACK CHRISTMAS CAROLS 2016

It was 19/12/2017 was a happiest moment to all. Watu mbalimbali wakiimba kama Kelvin Weber, KKKT Kimara, KKKT uinjilisti kijitonyama, RIVERS OF LIFE, NA pia wengine walifanya vichekesho kama Sam Sasali na Mc Pilipili.

MAGAZETI LEO 01.02.2017

ALIONGOZA MITIHANI YA FORM 4 MWAKA 2016 ASEMA HAYA.

Kinara wa Kidato cha Nne Nchini Afichua Siri ya Kufanya Vizuri,Adai ni Mungu na Wazazi Tu..!!!

Mwanafunzi wa kwanza katika matokeo ya kidato cha nne nchini kutoka shule ya Sekondari ya Feza Boys jijini Dar es Salaam, Alfred H. Shauri (katikati) akielelzea siri ya mafanikio yake kwa wanahabari.

MWANAFUNZI wa kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2016, Alfred H. Shauri, ameeleza siri ya mafaniko yake kuwa ilitokana na kusoma kwa bidii na kumtanguliza Mungu katika kila alichofanya.

Akizungumza na wanahabari katika Shule ya Sekondari ya Feza Boys alikosoma eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam, amesema kitu cha  kwanza katika kila alilofanya ni kumtanguliza Mungu katika masomo yake na cha pili alikuwa sambamba na wazazi wake kuhakikisha anachukua ushauri wao juu ya masomo yake ambapo kwa uapnde wa walimu wake alisema aliwasikilza kwa makini na kuwauliza maswali pale alipokuwa akihitaji msaada na kujisomea vitabu mbalimbali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Sekondari za Feza, Ibrahim Yunus,  alisema kuwa mafaniko ya mwanafunzi huyo yametokana na juhudi zake mwenyewe alizokuwa nazo wakati akiwa shuleni hapo kwani aliweza kuwa wa kwanza pia katika shindano la insha  iliyozikutanisha shule za Afrika Mashariki mwezi Mei mwaka jana.
Source: udakuspecially.com

MWANAFUNZI KINARA WA KIDATO CHA NNE 2016 ASEMA HAYA.

Kinara wa Kidato cha Nne Nchini Afichua Siri ya Kufanya Vizuri,Adai ni Mungu na Wazazi Tu..!!!

Mwanafunzi wa kwanza katika matokeo ya kidato cha nne nchini kutoka shule ya Sekondari ya Feza Boys jijini Dar es Salaam, Alfred H. Shauri (katikati) akielelzea siri ya mafanikio yake kwa wanahabari.

MWANAFUNZI wa kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2016, Alfred H. Shauri, ameeleza siri ya mafaniko yake kuwa ilitokana na kusoma kwa bidii na kumtanguliza Mungu katika kila alichofanya.

Akizungumza na wanahabari katika Shule ya Sekondari ya Feza Boys alikosoma eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam, amesema kitu cha  kwanza katika kila alilofanya ni kumtanguliza Mungu katika masomo yake na cha pili alikuwa sambamba na wazazi wake kuhakikisha anachukua ushauri wao juu ya masomo yake ambapo kwa uapnde wa walimu wake alisema aliwasikilza kwa makini na kuwauliza maswali pale alipokuwa akihitaji msaada na kujisomea vitabu mbalimbali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Sekondari za Feza, Ibrahim Yunus,  alisema kuwa mafaniko ya mwanafunzi huyo yametokana na juhudi zake mwenyewe alizokuwa nazo wakati akiwa shuleni hapo kwani aliweza kuwa wa kwanza pia katika shindano la insha  iliyozikutanisha shule za Afrika Mashariki mwezi Mei mwaka jana.
Source: udakuspecially.com

Jan 31, 2017

MAMA WA MASAUTI UPENDO NKONE:

UPENDO NKONE
"Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, ninawasalim sana katika Jina la Yesu. Napenda kumshukuru Mungu kwa neema yake maishani mwangu Amekuwa mtetezi wangu katika mengi , nampenda Yesu na nafurahi kuwa nae maishani mwangu. Napenda kuwashukuru funs wangu wote wanaonunua ,kusikiliza na kuzitizama kazi zangu , mmekua moja ya sababu zilizo fanya uchumi wangu kuinuka , I want to thank you and God bless you so much. Kwa sasa album nilizonazo ni tano 5, vol 1 - Mungu baba , vol 2 - Hapa nilipo, vol 3 - zipo faida, vol 4- uniongoze Yesu, vol 5- Omba Yesu anasikia. Kwasasa ninakuja na album mpya vol 6 ..... Ambayo January mwishoni itatoka . Jina la album nitawajulisheni. Nawashukuru wote ambao mmekua mkiniombea na kunipigia simu kunitia Moyo ndani na nje ya Tanzania, Thank you all. Naomba msiache kuniombea kwasababu nasikia kutumika kwa viwango vya juu zaidi.       Napenda kuwapa pole wale wote ambao wamepatwa na matatizo  misiba, magonjwa,kuanguka kiuchumi Nk poleni sana.                         Napenda Kuwatia Moyo kwa neno la Mungu kutoka  Yohana 6:37 ukimwendea Yesu na kuyatii maagizo yake, hawezi kukutupa nje , pamoja na magumu tulio nayo tusiache kimwendea atatuvusha tu. Nawatakia mwaka mpya mwema 2017 uwe ni mwaka mwema kwenu, mfarijiwe, muinuliwe , Mungu awape majibu ya mahitaji yenu. Nawapenda nyote. AMEN."

Jan 30, 2017

GAZETI LINALOTAKIWA KUOMBA RADHI MASAA 24 HILI HAPA.

Gazeti la Tanzania lililopewa saa 24 kumuomba radhi Rais Magufuli

Onyo limetoka kwenye Idara ya habari maelezo kupitia kwa Mkurugenzi wake Dr. Hassan Abbasi ambapo gazeti lililoandika kichwa cha habari ‘UFISADI NDANI YA OFISI YA JPM‘ limepewa saa 24 kuomba radhi.

Taarifa ya Idara hiyo imesema ‘licha ya habari hiyo kujenga dhana kuwa Rais John Pombe Magufuli anahusika na kinachoitwa ufisadi, msingi wa taarifa husika ni tatizo la manunuzi shirika la elimu Kibaha.

Kwa kuwa ni jambo lililodhahiri kuwa shirika la elimu Kibaha sio ofisi, Idara wala kitengo ndani ya Ofisi ya Rais, Mwandishi na Mhariri wa habari husika wamedhihirisha malengo ya kumchafua Rais binafsi kwa jamii.

Serikali inawaagiza Wahariri wa gazeti hilo kujitathmini na kuchukua hatua kwa kutumia kifungu cha 410 cha sheria ya huduma za habari 2016 kinachowapa fursa ya kuomba radhi, kwa kumuomba radhi Rais ndani ya saa 24 kuanzia saa kumi jioni ya January 30 2017.

Iwapo wahusika wataona muhali kufanya hivyo, Serikali itachukua hatua kali kwa mujibu wa sheria na masharti ya usajili wa gazeti husika, Tunaendelea kuwashukuru Wanahabari wanaofuata madili ya taaluma. – Dr. Hassan Abbasi.
Millard ayo.com

TD JAKES

February we are back with all new episodes all month long, starting February 2nd. Don't miss a moment! #TDJFebruary #TDJakesShow

Angalia hizi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...